CHELO SAGUTI

  • Home
  • News
  • Downloads
  • Internet
  • Health

Monday, January 13, 2014

Huyu ni mpagani wa kale sana anaitwa Nimrod

 Chelo     8:24 AM     5 comments   



 

Huyu ni mpagani wa kale sana anaitwa Nimrod. Wanatheolojia na wanahistoria wengi wa wanamhusisha moja kwa moja na ujenzi wa mnara wa babeli. Babilon ndio kitovu cha upagani ulimwenguni, mji huu upo Iraq(ya sasa) maili 90 kusini mwa mji wa Baghdad.

Nimrod alijenga hii Babiloni, akajenga na Ninawi, akaenda Siria akajenga mji wa Ashuri na aliijenga pia Kaanani.
Nimrod ametajwa mara 4 ndani ya biblia,mara tatu ametajwa moja kwa moja. katika Mwanzo 10:8-12 na ametajwa pia katika Mika 5:6 na Nyakati 1:10, katika Qur'an ametajwa katika sherehe ya tafsiri ya aya ya 258 ya sura ya pili(baqarah) kama"Namrudha".
Huyu aliabudiwa kama mungu, kutokana na ushujaa wake wa uwindaji, na watu wa zama hizo walimfuata kama msaada badala ya Mungu, aliwalinda dhidi ya wanyama wakali.
Kwa mujibu wa wanahistoria alimuoa mwanamke aitwae Semiramis, inasemekana alikuwa ni mke wa baba yake aitwae Kushi, mtu mweusi wa zama hizo, zamani kwao ilikuwa kawaida mtu kumrithi mke baba yake yaani kumuoa mama yake mzazi.
Nimrodi alijiita mungu na aliabudiwa,alitaka kushindana na Mungu kwa kujenga mnara wa babeli,inasemekana aliona katika mbingu kipande cha nguo nyeusi na taji, akaamuru atengenezewe taji kama hilo na akawa mfalme wa kwanza ulimwenguni kuvaa taji, wasiojua kuhusu hilo walidai ameshushiwa toka mbinguni.
Nimrodi ana historia nyingi sana kwani aliishi miaka mingi lakini habari zake nyingi zilipindishwa na kutiwa chumvi na kukosewa kadiri muda ulivyosogea kuja karne zetu! alikuwa mkuu wa uwindaji na hodari "mighty hunter" na amekuwa wa kwanza akiitwa "mighty" tangu mafuriko ya Nuhu kutokea.
Biblia haitaji kuhusu mama yake(semiramis) au tarehe ya kuzaliwa Nimrod lakini masalia ya kumbukumbu za Wamisri na wababeli vinamtaja semiramis kuwa mama yake na Nimrod kuzaliwa december 25 inayosheherekewa Christmass leo!
Biblia wala Qur'an havitaji kifo cha Nimrod, lakini vitabu vya kale zaidi ya hivyo vinasema alikufa kifo kibaya sana,wengine wanasema aliuawa na mnyama mwitu na wengine wakadai Shemu alimwua kwa sababu aliwapelekea watu kuabudu ibada ya Baal.
Mama-mke (Semiramis) alimfanya mwanae au mumewe kuwa mungu baada ya kifo chake, na yeye alijipa uungu mke(goddess). alizaa mtoto kwa zinaa na kumuita Tamuzi akawa mwindaji hodari na pia mungu wa mavuno.Tamuzi alioa mke aitwae Ishtar kwa kigiriki Jupiter.
Nimrod akawa mungu baba, Semilamis mungu mama, na Tamuzi mungu mwana na mungu wa mavuno. nadharia ya imani hizi za kipagani zilianzia hapo.
Wanahistoria wanasema tamuzi alikuwa kipenzi cha wanawake sana(ezekieli 8:14),kifo cha Tamuzi kilitokea mawindoni, japo kuna utata kuhusu hilo! wengi wanadai aliuawa na nguruwe hivyo mama yake aliamuru wafuasi wale nguruwe sana kama sehemu ya kisasi...........
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Newer Post Older Post Home

5 comments:

  1. jobsAugust 27, 2019 at 3:03 PM

    Pia fuatilia link hii ujue MNARA WA BABELI kwasasa ni upi https://wingulamashahidi.org/2018/09/11/mnara-wa-babeli/

    ReplyDelete
    Replies
      Reply
  2. UnknownDecember 24, 2019 at 9:20 PM

    UBARIKIWE NA MUNGU KWA MAFUNDISHO NAKUOMBEA MUNGU ANAE JUWA AKILI ZETU UKUJAZIE FEHEMA NA NEEEMA KWAWAELIMISHA HAWA WAJUKUU WA NIMRODI,

    ReplyDelete
    Replies
      Reply
  3. UnknownApril 3, 2020 at 7:50 AM

    Ubarikiwe

    ReplyDelete
    Replies
      Reply
  4. UnknownJune 5, 2020 at 2:52 PM

    Og bob

    ReplyDelete
    Replies
      Reply
  5. UnknownJuly 29, 2020 at 1:29 PM

    Tante

    ReplyDelete
    Replies
      Reply
Add comment
Load more...

Popular Posts

  • Huyu ni mpagani wa kale sana anaitwa Nimrod
      Huyu ni mpagani wa kale sana anaitwa Nimrod . Wanatheolojia na wanahistoria wengi wa wanamhusisha moja kwa moja na ujenzi wa mnara ...
  • HAYA SASA WALE WADADA CHEKI MITINDO MIPYA YA MISHONO MAGAUNI NA SKETI
    Chelo Saguti anakuletea kipengele kingine tena maalumu kwa ajili ya mitindo ya mavazi mwanamke upendeze kitenge ndio asili yetu,, MIT...
  • UNAMFAHAMU MANSA MUSA? BINADAMU TAJIRI ALIYEPATA KUISHI MIAKA YA 1280 -1337
    UNAMFAHAMU MANSA MUSA? BINADAMU TAJIRI ALIYEPATA KUISHI? Mimi binafsi napenda kumuita Mansa Kankan Musa I, alipata kuishi mwaka 1280 hadi ...
  • (no title)
    OK.. Anaitwa Genghis Khan.. yasadikika alizaliwa mwaka 1162 na kufariki 1227! alipozaliwa aliitwa Temujin! Temujin au Genghis khan alikuwa...

Total Pageviews

Powered by Blogger.

About Me

My Photo
Chelo
View my complete profile

Followers

Featured Posts

Copyright © CHELO SAGUTI | Powered by Blogger