Anaitwa Genghis Khan.. yasadikika alizaliwa mwaka 1162 na kufariki 1227! alipozaliwa aliitwa Temujin!
Temujin au Genghis khan alikuwa ni kiongozi aliyeanzisha dola kuu ya Mongolia na kuwa dola kubwa iliyomiliki sehemu nyingi za ulaya mashariki na Asia ikiwemo China na Russia.. aliweza kupata mafanikio baada ya kupiga makabila yote ya mongolia na kuyaweka chini yake.. machifu na viongozi wote walipoteza madaraka yao na utawala kuwa chini yake, hivyo akapewa jina la Chingis Khan/ Genghis Khan yaani "universal ruler".
Genghis anasadikika kuwa ni mmoja kati ya watu katili na wabaya zaidi katika historia ya ulimwengu. Mamilioni ya watu wamekufa chini ya amri yake na mkono wake.
Kuna uzushi ya kuwa Genghis ameua watu milioni moja laki saba na elfu arobaini na nane(1,748,000) kwa saa moja... Ni UONGO!
ILA, hiyo inakadiriwa kuwa ni idadi ya watu waliokuwa wakiishi katika mji wa Persia wa Nishapur uliopo Iran ya sasa..
Mkwe wake kipenzi (aliyemuoa mtoto wake wa kike) aliyeitwa Toquchar alipigwa mshale na mtu mkazi wa Nishapur, hiyo ilimkasirisha mtoto wake na kuamuru watu wote wa Nishapur wauawe... Majeshi ya Genghis yaliua watu wote ikiwemo na mifugo! ni wachache waliosalia... Ila sio Genghis kuua kwa saa moja kwa mkono wake!!
Mongolia inamuenzi leo, Genghis kama baba wa taifa lao!! korea, China zote zinamuelewa mtu huyu aliyepata kutikisa enzi za utawala wake.
Kwakuwa alikuwa anasafiri sana na alikuwa kipenzi cha wanawake, inasemekana alizaa sana kila mahali... 2003 study record, inaonesha kwamba, watu milioni 16 walio hai ulimwenguni wanatokana na kizazi chake, yaani 0.6% ya watu duniani ni uzawa wa Genghis Khan...
Huyo ndio mtawala wa Dunia kabla ya watawala tuliowashuhudia kwa macho....
0 comments:
Post a Comment