Huyu ni mpagani wa kale sana anaitwa Nimrod. Wanatheolojia na wanahistoria wengi wa wanamhusisha moja kwa moja na ujenzi wa mnara wa babeli. Babilon ndio kitovu cha upagani ulimwenguni, mji huu upo Iraq(ya sasa) maili 90 kusini mwa mji wa Baghdad.
Nimrod alijenga hii Babiloni, akajenga na Ninawi, akaenda Siria akajenga mji wa Ashuri na aliijenga pia Kaanani. Nimrod ametajwa mara 4 ndani ya biblia,mara tatu ametajwa moja kwa moja. katika Mwanzo 10:8-12 na ametajwa pia katika Mika 5:6 na Nyakati 1:10, katika Qur'an ametajwa katika sherehe ya tafsiri ya aya ya 258 ya sura ya pili(baqarah) kama"Namrudha". Huyu aliabudiwa kama mungu, kutokana na ushujaa wake wa uwindaji, na watu wa zama hizo walimfuata kama msaada badala ya Mungu, aliwalinda dhidi ya wanyama wakali. Kwa mujibu wa wanahistoria alimuoa mwanamke aitwae Semiramis, inasemekana alikuwa ni mke wa baba yake aitwae Kushi, mtu mweusi wa zama hizo, zamani kwao ilikuwa kawaida mtu kumrithi mke baba yake yaani kumuoa mama yake mzazi. Nimrodi alijiita mungu na aliabudiwa,alitaka kushindana na Mungu kwa kujenga mnara wa babeli,inasemekana aliona katika mbingu kipande cha nguo nyeusi na taji, akaamuru atengenezewe taji kama hilo na akawa mfalme wa kwanza ulimwenguni kuvaa taji, wasiojua kuhusu hilo walidai ameshushiwa toka mbinguni. Nimrodi ana historia nyingi sana kwani aliishi miaka mingi lakini habari zake nyingi zilipindishwa na kutiwa chumvi na kukosewa kadiri muda ulivyosogea kuja karne zetu! alikuwa mkuu wa uwindaji na hodari "mighty hunter" na amekuwa wa kwanza akiitwa "mighty" tangu mafuriko ya Nuhu kutokea. Biblia haitaji kuhusu mama yake(semiramis) au tarehe ya kuzaliwa Nimrod lakini masalia ya kumbukumbu za Wamisri na wababeli vinamtaja semiramis kuwa mama yake na Nimrod kuzaliwa december 25 inayosheherekewa Christmass leo! Biblia wala Qur'an havitaji kifo cha Nimrod, lakini vitabu vya kale zaidi ya hivyo vinasema alikufa kifo kibaya sana,wengine wanasema aliuawa na mnyama mwitu na wengine wakadai Shemu alimwua kwa sababu aliwapelekea watu kuabudu ibada ya Baal. Mama-mke (Semiramis) alimfanya mwanae au mumewe kuwa mungu baada ya kifo chake, na yeye alijipa uungu mke(goddess). alizaa mtoto kwa zinaa na kumuita Tamuzi akawa mwindaji hodari na pia mungu wa mavuno.Tamuzi alioa mke aitwae Ishtar kwa kigiriki Jupiter. Nimrod akawa mungu baba, Semilamis mungu mama, na Tamuzi mungu mwana na mungu wa mavuno. nadharia ya imani hizi za kipagani zilianzia hapo. Wanahistoria wanasema tamuzi alikuwa kipenzi cha wanawake sana(ezekieli 8:14),kifo cha Tamuzi kilitokea mawindoni, japo kuna utata kuhusu hilo! wengi wanadai aliuawa na nguruwe hivyo mama yake aliamuru wafuasi wale nguruwe sana kama sehemu ya kisasi...........
OK.. Anaitwa Genghis Khan.. yasadikika alizaliwa mwaka 1162 na kufariki 1227! alipozaliwa aliitwa Temujin! Temujin au Genghis khan alikuwa ni kiongozi aliyeanzisha dola kuu ya Mongolia na kuwa dola kubwa iliyomiliki sehemu nyingi za ulaya mashariki na Asia ikiwemo China na Russia.. aliweza kupata mafanikio baada ya kupiga makabila yote ya mongolia na kuyaweka chini yake.. machifu na viongozi wote walipoteza madaraka yao na utawala kuwa chini yake, hivyo akapewa jina la Chingis Khan/ Genghis Khan yaani "universal ruler". Genghis anasadikika kuwa ni mmoja kati ya watu katili na wabaya zaidi katika historia ya ulimwengu. Mamilioni ya watu wamekufa chini ya amri yake na mkono wake.
Kuna uzushi ya kuwa Genghis ameua watu milioni moja laki saba na elfu arobaini na nane(1,748,000) kwa saa moja... Ni UONGO! ILA, hiyo inakadiriwa kuwa ni idadi ya watu waliokuwa wakiishi katika mji wa Persia wa Nishapur uliopo Iran ya sasa.. Mkwe wake kipenzi (aliyemuoa mtoto wake wa kike) aliyeitwa Toquchar alipigwa mshale na mtu mkazi wa Nishapur, hiyo ilimkasirisha mtoto wake na kuamuru watu wote wa Nishapur wauawe... Majeshi ya Genghis yaliua watu wote ikiwemo na mifugo! ni wachache waliosalia... Ila sio Genghis kuua kwa saa moja kwa mkono wake!! Mongolia inamuenzi leo, Genghis kama baba wa taifa lao!! korea, China zote zinamuelewa mtu huyu aliyepata kutikisa enzi za utawala wake.
Kwakuwa alikuwa anasafiri sana na alikuwa kipenzi cha wanawake, inasemekana alizaa sana kila mahali... 2003 study record, inaonesha kwamba, watu milioni 16 walio hai ulimwenguni wanatokana na kizazi chake, yaani 0.6% ya watu duniani ni uzawa wa Genghis Khan... Huyo ndio mtawala wa Dunia kabla ya watawala tuliowashuhudia kwa macho....
UNAMFAHAMU MANSA MUSA? BINADAMU TAJIRI ALIYEPATA KUISHI?
Mimi binafsi napenda kumuita Mansa Kankan Musa I, alipata kuishi mwaka 1280 hadi mwaka 1337 japo kuna vyanzo vingine vimekataa hilo na kudai alifariki mapema zaidi.. Mansa Musa I anasadikika kuwa miongoni mwa watu tajiri zaidi katika historia! mtupilie mbali J.D. Rockerfeller! Mansa Musa, alipata kuwa "mansa" yaani mfalme wa wafalme, katika ufalme mkubwa wa afrika ya kabla ya ukoloni ulioanzishwa na mtu aliyepata kuitwa Sundiata Keita, "Malike Empire" au Mali Empire.
Mansa Musa aliweza kuudhihirishia ulimwengu na ni kielelezo tosha cha kuonesha kwamba afrika sio bara masikini na halikuwa bara giza, mnamo mwaka 1324 alipoenda kuzuru makkah kwa ajili ya ibada ya waisilamu ya hijja!
Mansa Musa alifanya safari ya KIHISTORIA iliyobaki kuwa mazungumzo kwa wanafunzi wa historia hadi leo hii, kwa kuonesha fahari iliyotukuka ya ardhi ya neema ya madini ya Mali kwa kubeba waungwana 60,000 pamoja na watumwa 12,000 pamoja nae ambao walibeba pound 4 za dhahabu kila mmoja na ndani ya msafara kulikuwa na ngamia 80 waliokuwa wamevishwa mavazi ya thamani na kubebeshwa mifuko ya unga wa dhahabu kadiri ya pound 50 kwa 300 kila mmoja..
Mansa Musa alipita akigawa dhahabu kwa masikini kuanzia Mali hadi Misri alipotua, kisha kuvuka maji na kuingia saudia akiwa amejizatiti.. aliweza kuzifanya nchi za Saudia na Misri kushuka kiuchumi hadi anakufa, miaka kumi na kitu baadae, kwani bei ya dhahabu ilishuka sana na kupoteza thamani kwani ilikuwa ya kumwagaa!! Alitoa kiasi kikubwa zaidi cha pesa kama zawadi kwa Sultan wa wakati huo wa Misri na Saudia. pia katika safari yake hiyo aliweza kujenga misikiti kila alipokuwa njiani ilikuwa ni desturi yake kujenga misikiti kila ijumaa, baadhi ya misikiti ambayo ipo hadi leo hii! Musa alirithi ufalme kutoka kwa Abubakari II ambaye alikufa maji katika bahari ya atlantic alipojaribu kuvuka kuona upande wa pili wa dunia, akiwa na boti zaidi ya mia mbili!! zilizosheheni vyakula na maji kwa ajili ya safari ya miaka kadhaa kufika mwisho wa bahariii.............!! Jina mansa musa sio jina geni hata kabla ya maijilio ya wazungu, wana historia wengi kama Ibn Battuta wamemuelezea Mansa Musa hata kabla ya ukoloni mkongwe....Arabia, Europa, Israel na west Indies wote wameandika vitabu na vitabu juu ya tajiri huyu......... Lakini Propaganda za wengi zimefanya nchi kama Mali, leo hii ni ya kupewa misaada kwa sababu ya machafuko ya kushinikiza..hii ni nchi iliyotukuka hata kabla ya kugundulika bara la Amerika karne ya 15. NANI ANASEMA AFRIKA TULIKUWA MANYANI KABLA YA WAZUNGU? NANI ANASEMA AFRIKA HAINA HISTORIA ZAIDI YA GIZA? NANI ANASEMA AFRIKA HAIKUWA NA MAENDELEO? NANI ANASEMA TULISHINDWA KUJITAWALA? NANI ANASEMA HATUKUTAMBULIKA DUNIANI? NANI ANYOOSHE KIDOLE..........!!! Jifunze maarifa ya ukweli!!